Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua msamiati uliotumiwa katika hadithi ili kuwezesha ufahamu,
  2. kusikiliza hadithi ikisomwa na mwalimu kuhusu shughuli za dukani ili kuimarisha stadi ya kusikiliza,
  3. kusoma hadithi kuhusu dukani kwa ufasaha ili kujenga usomaji bora,
  4. kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa kuhusu shughuli za dukani ili kupata ujumbe,

g) kuthamini biashara maishani kama njia moja ya kujitegemea maishani. 

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

• Mwanafunzi asikilize mwalimu akisoma hadithi ya mwalimu na baadaye kuuliza na kujibu maswali.

  • Mwanafunzi asome pamoja na wengine darasani, kisha wasome wawili wawili na baadaye asome peke yake.
  • Mwanafunzi ajadili picha kwenye hadithi.
  • Mwanafunzi atabiri kuhusu kitakachotokea katika hadithi wakiwa wawili wawili.
  • Mwanafunzi ashirikiane na wengine kujadili msamiati uliotumika katika hadithi.
  • Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi husika ikisomwa kupitia kinasasauti na kisha kuijadili.
  • Mwanafunzi aweza kutazama video ya mtu mzima au mtoto akisoma hadithi husika kwa ufasaha kisha aige usomi ule.
  • Wanafunzi waweza kusomeana hadithi katika vikundi.
  • Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyosoma
  • Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali.
  • Mwanafunzi ashiriki kujadili baadhi ya maswali darasani,  katika vikundi au wakiwa wawili wawili.

MASWALI DADISI

1) Umewahi kusoma hadithi gani kuhusu dukani?

2) Je, ni hadithi gani iliyokufurahisha sana?

 Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza ubunifu – unadhihirishwa na usimulizi na utungaji wa sentensi.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

Elimu ya maendeleo endelevu: elimu ya maswala ya kifedha katika ujuzi wa kutumia pesa vizuri.

stadi za maisha – Kuwa na ujasiri wa kwenda na kufanya maamuzi mwafaka ya ununuzi.

Uhusiano na masomo mengine: Mathematics Activities na English Activitites.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kushiriki katika maigizo ya shughuli za dukani shuleni kushiriki katika majadiliano kuhusu bidhaa zinazopatikana dukani.

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji Kuweza kuwa mwadilifu katika matumizi ya pesa dukani.

ushirikiano – Kufanya kazi katika vikundi.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kuweza kutumwa dukani na wazazi na kutumia pesa inavyofaa.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuchunguza anavyotumia msamiati wa dukani katika mawasiliano 
  • kuchunguza anavyotumia alama ya kuuliza katika mawasiliano
  • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
  • kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa
  • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi

• kufuatilia mwandiko wake.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatambua na kutumia msamiati wa dukani ipasavyo
  • anasimulia kisa kuhusu shughuli za dukani kwa ubunifu na ufasaha
  • anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani kwa ufasaha na ukakamavu
  • anafahamu kwa wepesi anayosoma au kusomewa
  • anatumia alama ya kuuliza katika maandishi kila inapohitajika
  • anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, kwa hati nadhifu na kwa kasi ifaayo.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatambua msamiati wa dukani
  • anasimulia kisa kuhusu shughuli za dukani kwa ufasaha
  • anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani kwa ufasaha
  • anafahamu anayosoma au kusomewa
  • anatumia alama ya kuuliza katika maandishi
  • anaandika kisa kwa mtiririko na kwa hati bora.

 Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatambua baadhi ya msamiati wa dukani.
  • anasimulia kisa kuhusu shughuli za dukani
  • anasoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani 
  • anafahamu  baadhi ya mambo anayosoma au kusomewa
  • anatumia alama ya kuuliza katika baadhi ya sentensi
  • anaandika kisa kwa hati zinazosomeka. 

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutambua baadhi ya msamiati wa dukani
  • ana changamoto katika kusimulia kisa kuhusu shughuli za dukani 
  • ana changamoto katika kusoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani 
  • ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma au kusomewa
  • ana changamoto katika kuakifisha sentensi kwa kutumia alama ya kuuliza

ana changamoto katika kuandika kisa kuhusu mada aliyofunzwa. 

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *