Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada ili kujenga stadi ya uandishi,
  2. kufurahia uandishi wa visa tofauti ili kuimarisha mawasiliano andishi.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

  • Mwanafunzi apewe hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka.
  • Mwanafunzi aeleze yaliyo muhimu katika uandishi

k.v. mwandiko nadhifu, maudhui, mtiririko n.k.

  • Mwanafunzi asome kielelezo cha kisa kilichoandikwa na mwanafunzi au mtu sliye na umahiri katika uandishi.
  • Wanafunzi waweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili.
  • Mwanafunzi aandike kisa kifupi kinachohusiana na mada. Kisa hiki kifuate hatua tano za uandishi:

maandalizi, nakala ya kwanza, marejeleo, uhariri na uchapishaji. 

MASWALI DADISI

  1. Je, ni mambo yapi yanayofaa kuzingatiwa unapoandika kisa?
  2. Je, ni mambo gani utakayoshughulikia ukiandika kuhusu dukani?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza ubunifu – unadhihirishwa na usimulizi na utungaji wa sentensi.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

Elimu ya maendeleo endelevu: elimu ya maswala ya kifedha katika ujuzi wa kutumia pesa vizuri.

stadi za maisha – Kuwa na ujasiri wa kwenda na kufanya maamuzi mwafaka ya ununuzi.

Uhusiano na masomo mengine: Mathematics Activities na English Activitites.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kushiriki katika maigizo ya shughuli za dukani shuleni kushiriki katika majadiliano kuhusu bidhaa zinazopatikana dukani.

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji Kuweza kuwa mwadilifu katika matumizi ya pesa dukani.

ushirikiano – Kufanya kazi katika vikundi.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kuweza kutumwa dukani na wazazi na kutumia pesa inavyofaa.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuchunguza anavyotumia msamiati wa dukani katika mawasiliano 
  • kuchunguza anavyotumia alama ya kuuliza katika mawasiliano
  • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
  • kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa
  • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi

• kufuatilia mwandiko wake.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatambua na kutumia msamiati wa dukani ipasavyo
  • anasimulia kisa kuhusu shughuli za dukani kwa ubunifu na ufasaha
  • anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani kwa ufasaha na ukakamavu
  • anafahamu kwa wepesi anayosoma au kusomewa
  • anatumia alama ya kuuliza katika maandishi kila inapohitajika
  • anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, kwa hati nadhifu na kwa kasi ifaayo.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatambua msamiati wa dukani
  • anasimulia kisa kuhusu shughuli za dukani kwa ufasaha
  • anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani kwa ufasaha
  • anafahamu anayosoma au kusomewa
  • anatumia alama ya kuuliza katika maandishi
  • anaandika kisa kwa mtiririko na kwa hati bora.

 Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatambua baadhi ya msamiati wa dukani.
  • anasimulia kisa kuhusu shughuli za dukani
  • anasoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani 
  • anafahamu  baadhi ya mambo anayosoma au kusomewa
  • anatumia alama ya kuuliza katika baadhi ya sentensi
  • anaandika kisa kwa hati zinazosomeka. 

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutambua baadhi ya msamiati wa dukani
  • ana changamoto katika kusimulia kisa kuhusu shughuli za dukani 
  • ana changamoto katika kusoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani 
  • ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma au kusomewa
  • ana changamoto katika kuakifisha sentensi kwa kutumia alama ya kuuliza
  • ana changamoto katika kuandika kisa kuhusu mada aliyofunzwa. 

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *