MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua matumizi ya alama ya kuuliza (?) katika kuimarisha mawasiliano,
- kusoma sentensi zilizo na matumizi ya alama ya kuuliza (?) katika kuimarisha stadi ya
kusoma,
- kuandika sentensi akitumia alama ya kuuliza (?) katika kuimarisha stadi ya kuandika,
- kuthamini matumizi ya alama ya kuuliza (?) katika mawasiliano.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi aandike alama ya kuuliza (?).
- Mwanafunzi afafanue matumizi ya alama ya kuuliza (?).
- Mwanafunzi atunge sentensi akitumia alama ya kuuliza (?).
- Mwanafunzi asome sentensi zilizo na alama ya kuuliza (?).
- Wanafunzi waweza kushirikishwa kusoma sentensi zinazotumia alama ya kuuliza (?) wakiwa wawili wawili au katika vikundi.
- Mwanafunzi aandike sentensi akitumia alama ya kuuliza (?).
MASWALI DADISI
- Je, alama (?) huitwaje?
- Je, utatumia alama (?) unapofanya nini?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza ubunifu – unadhihirishwa na usimulizi na utungaji wa sentensi.
Uhusiano na masuala mtambuko:
Elimu ya maendeleo endelevu: elimu ya maswala ya kifedha katika ujuzi wa kutumia pesa vizuri.
stadi za maisha – Kuwa na ujasiri wa kwenda na kufanya maamuzi mwafaka ya ununuzi.
Uhusiano na masomo mengine: Mathematics Activities na English Activitites.
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kushiriki katika maigizo ya shughuli za dukani shuleni kushiriki katika majadiliano kuhusu bidhaa zinazopatikana dukani.
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji – Kuweza kuwa mwadilifu katika matumizi ya pesa dukani.
ushirikiano – Kufanya kazi katika vikundi.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kuweza kutumwa dukani na wazazi na kutumia pesa inavyofaa.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza anavyotumia msamiati wa dukani katika mawasiliano
- kuchunguza anavyotumia alama ya kuuliza katika mawasiliano
- kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa
- kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
• kufuatilia mwandiko wake.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua na kutumia msamiati wa dukani ipasavyo
- anasimulia kisa kuhusu shughuli za dukani kwa ubunifu na ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani kwa ufasaha na ukakamavu
- anafahamu kwa wepesi anayosoma au kusomewa
- anatumia alama ya kuuliza katika maandishi kila inapohitajika
- anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, kwa hati nadhifu na kwa kasi ifaayo.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua msamiati wa dukani
- anasimulia kisa kuhusu shughuli za dukani kwa ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani kwa ufasaha
- anafahamu anayosoma au kusomewa
- anatumia alama ya kuuliza katika maandishi
- anaandika kisa kwa mtiririko na kwa hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua baadhi ya msamiati wa dukani.
- anasimulia kisa kuhusu shughuli za dukani
- anasoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani
- anafahamu baadhi ya mambo anayosoma au kusomewa
- anatumia alama ya kuuliza katika baadhi ya sentensi
- anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutambua baadhi ya msamiati wa dukani
- ana changamoto katika kusimulia kisa kuhusu shughuli za dukani
- ana changamoto katika kusoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani
- ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma au kusomewa
- ana changamoto katika kuakifisha sentensi kwa kutumia alama ya kuuliza
ana changamoto katika kuandika kisa kuhusu mada aliyofunzwa.