MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutaja majina ya ndege mbalimbali ili kuimarisha stadi ya kuzungumza,
- kutambua msamiati unaotumiwa katika kutunza ndege ili kuimarisha mawasiliano,
- kutumia majina ya ndege katika sentensi sahihi ili kuwezesha mazungumzo,
- kutumia msamiati wa kutunza ndege katika sentensi ili kuwezesha mazungumzo,
- kusoma maneno na sentensi kuhusu ndege ampendaye ili kujenga usomaji bora,
- kuandika maneno na sentensi kuhusu ndege ampendaye ili kujenga uandishi bora,
- kuthamini utunzaji wa ndege ampendaye.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi atazame picha na kuwatambua ndege tofauti tofauti.
- Mwanafunzi atunge sentensi sahihi kwa kutumia msamiati kuhusu ndege.
- Mwanafunzi atoe maana ya msamiati unaotumiwa katika kutunza ndege.
- Mwanafunzi achore baadhi ya ndege.
- Mwanafunzi aweza kutazama video ya utunzaji wa ndege.
- Mwanafunzi atazame michoro na picha za ndege wa nyumbani wakitunzwa.
- Mwanafunzi asome maneno na sentensi katika kadi na chati kuhusu ndege.
- Mwanafunzi aandike majina na sentensi kuhusu ndege.
MASWALI DADISI
- Ni ndege wepi wanaofugwa?
- Unamtunzaje ndege umpendaye?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi na wakiwa wawili wawili ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza hadithi, msamiati na sauti kufikiri kwa kina – kung’amua sifa za ndege ampendaye
Uhusiano na masuala mtambuko:
elimu ya maendeleo endelevu (masilahi ya wanyama – kujali na kutunza ndege)
Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities na English Activitites.
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kushiriki katika vikundi shuleni kama vile chama cha ukulima kuimba na kukariri mashairi kuhusu ndege wa nyumbani.
Uhusiano na Maadili:
upendo kwa ndege wanaofugwa uwajibikaji katika kutunza ndege.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kutunza ndege na wanyama.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza anavyotumia msamiati wa ndege wanaofugwa katika mawasiliano
- kuchunguza anavyotumia juu ya na chini ya katika mawasiliano
- kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
- kufuatilia mwandiko wake.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anasikiliza na kusimulia hadithi kwa ukakamavu na ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye kwa wepesi na ufasaha
- anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
- anatumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi zenye ubunifu wa hali ya juu
- anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, hati nadhifu na kwa haraka.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anasikiliza na kusimulia hadithi kwa ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye kwa ufasaha
- anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- anatumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi
- anaandika kisa kwa
mtiririko na hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anasikiliza na kusimulia hadithi
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye
- anafahamu baadhi ya hadithi aliyosoma na kusomewa
- ana changamoto katika kutumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi
- anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kusimulia hadithi
- ana changamoto katika kusoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye
- ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- ana changamoto katika kutumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi
- ana changamoto katika kuandika kisa.