MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutaja aina za ndege wa nyumbani anaowajua ili kujenga stadi ya kuzungumza,
- kumtambua ndege ampendaye ili kujenga stadi ya kuzungumza,
- kusimulia kuhusu ndege ampendaye ili kujenga stadi ya kuzungumza,
- kusimulia kuhusu jinsi ndege ampendaye anavyotunzwa ili kujenga stadi ya kuzungumza,
- kusikiliza kwa makini masimulizi kuhusu utunzaji wa ndege wa nyumbani ili kujenga usikivu,
- kuthamini ndege wa nyumbani
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi ataje aina za ndege anaowajua.
- Mwanafunzi atambue ndege ampendaye.
- Mwanafunzi asimulie kuhusu ndege ampendaye katika darasa zima, wakiwa wawili wawili na katika vikundi.
- Mwanafunzi atazame picha za ndege mbalimbali wa nyumbani ili awatambue.
- Mwanafunzi aweza kutazama video na picha zinazoashiria utunzaji wa ndege mbalimbali.
- Mwanafunzi asimulie jinsi ya kutunza ndege kupitia kwa mgeni mwalikwa.
- Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu jinsi ndege ampendaye anavyotunzwa.
Wanafunzi waweza kushirikishwa kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu ndege wawapendao.
MASWALI DADISI
- Ni ndege gani umpendaye?
- Kwa nini unampenda ndege huyo?
- Unamtunzaje ndege umpendaye?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi na wakiwa wawili wawili ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza hadithi, msamiati na sauti kufikiri kwa kina – kung’amua sifa za ndege ampendaye
Uhusiano na masuala mtambuko:
elimu ya maendeleo endelevu (masilahi ya wanyama – kujali na kutunza ndege)
Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities na English Activitites.
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kushiriki katika vikundi shuleni kama vile chama cha ukulima kuimba na kukariri mashairi kuhusu ndege wa nyumbani.
Uhusiano na Maadili:
upendo kwa ndege wanaofugwa uwajibikaji katika kutunza ndege.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kutunza ndege na wanyama.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza anavyotumia msamiati wa ndege wanaofugwa katika mawasiliano
- kuchunguza anavyotumia juu ya na chini ya katika mawasiliano
- kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
- kufuatilia mwandiko wake.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anasikiliza na kusimulia hadithi kwa ukakamavu na ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye kwa wepesi na ufasaha
- anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
- anatumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi zenye ubunifu wa hali ya juu
- anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, hati nadhifu na kwa haraka.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anasikiliza na kusimulia hadithi kwa ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye kwa ufasaha
- anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- anatumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi
- anaandika kisa kwa
mtiririko na hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anasikiliza na kusimulia hadithi
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye
- anafahamu baadhi ya hadithi aliyosoma na kusomewa
- ana changamoto katika kutumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi
- anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kusimulia hadithi
- ana changamoto katika kusoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye
- ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- ana changamoto katika kutumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi
- ana changamoto katika kuandika kisa.