Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

 1. kutambua msamiati uliotumiwa katika hadithi aliyosoma au kusomewa ili kuimarisha ufahamu,
 2. kusoma hadithi zinazohusu ndege wa nyumbani ili kujenga usomaji bora,
 3. kusikiliza hadithi zinazohusu ndege wa nyumbani  zikisomwa ili kujenga usikivu,
 4. kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa kuhusu ndege  wanaofugwa ili kupata ujumbe,
 5. kuchangamkia kusoma hadithi ili kuendeleza ari ya kusoma zaidi. 

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

 • Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
 • Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
 • Mwanafunzi athibitishe utabiri wao baada ya kusoma hadithi.
 • Mwanafunzi ashiriki katika kusoma darasani, wakiwa wawili na baadaye asome peke yake.
 • Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ya mwalimu au hadithi iliyorekodiwa. 
 • Wanafunzi waweza kusomeana hadithi wakiwa wawili wawili au katika vikundi.
 • Wanafunzi waweza  kusoma  hadithi kwa kutumia vifaa vya kiteknolojia k.v. tarakilishi na projekta.
 • Mwanafunzi atunge sentensi akitumia msamiati  uliotumiwa katika hadithi.
 • Mwanafunzi anakili majina na sentensi zinazojumuisha majina ndege wa nyumbani. 
 • Mwanafunzi aweza  kusoma hadithi kwa kutumia jitabu lililowekwa mbele ya darasa. 
 • Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kutokana na hadithi.

MASWALI DADISI

 1. Ni nini unachokiona katika picha?
 2. Unafikiri ni nini  kitakachotokea katika hadithi?
 3. Unakumbuka nini kutokana na hadithi uliyosoma?
 4. Ni kwa nini unampenda ndege wako?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:  mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi na wakiwa wawili wawili ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza hadithi, msamiati na sauti kufikiri kwa kina – kung’amua sifa za ndege ampendaye

Uhusiano na masuala mtambuko: 

elimu ya maendeleo endelevu (masilahi ya wanyama – kujali na kutunza ndege)

Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities na English Activitites.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kushiriki katika vikundi shuleni kama vile chama cha ukulima kuimba na kukariri mashairi kuhusu ndege wa nyumbani.

Uhusiano na Maadili: 

upendo kwa ndege wanaofugwa uwajibikaji katika kutunza ndege.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kutunza ndege na wanyama.

Mapendekezo ya Tathmini:

 • kuchunguza anavyotumia msamiati wa ndege wanaofugwa katika mawasiliano 
 • kuchunguza anavyotumia juu ya na chini ya katika mawasiliano
 • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
 • kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
 • kufuatilia mwandiko wake.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

 • anasikiliza na kusimulia hadithi kwa ukakamavu na ufasaha
 • anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye kwa wepesi na ufasaha
 • anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
 • anatumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi zenye ubunifu wa hali ya juu
 • anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, hati nadhifu na kwa haraka.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anasikiliza na kusimulia hadithi kwa ufasaha
 • anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye kwa ufasaha
 • anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
 • anatumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi
 • anaandika kisa kwa

mtiririko na hati bora.

 Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anasikiliza na kusimulia hadithi
 • anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye 
 • anafahamu baadhi ya hadithi aliyosoma na kusomewa
 • ana changamoto katika kutumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi
 • anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.

 Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

 • ana changamoto katika kusimulia hadithi
 • ana changamoto katika kusoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye 
 • ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
 • ana changamoto katika kutumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi

ana changamoto katika kuandika kisa.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *