MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada ili kujenga stadi ya uandishi,
- kufurahia uandishi wa visa tofauti ili kuimarisha mawasiliano andishi.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi apewe hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka.
- Mwanafunzi aeleze yaliyo muhimu katika uandishi kama vile mwandiko nadhifu, maudhui, mtiririko n.k.
- Mwanafunzi asome kielelezo cha kisa kilichoandikwa na mwanafunzi au mtu mwingine aliye na umahiri katika uandishi.
- Wanafunzi waweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili.
• Mwanafunzi aandike kisa kifupi kinachohusiana na mada. Kisa hiki kifuate hatua tano za uandishi:
maandalizi, nakala ya kwanza, marejeleo, uhariri na uchapishaji.
MASWALI DADISI
- Je, ni mambo yapi yanayofaa kuzingatiwa unapoandika kisa?
- Je, unaweza kuandika kisa gani kinachohusiana na ndege umpendaye?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi na wakiwa wawili wawili ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza hadithi, msamiati na sauti kufikiri kwa kina – kung’amua sifa za ndege ampendaye
Uhusiano na masuala mtambuko:
elimu ya maendeleo endelevu (masilahi ya wanyama – kujali na kutunza ndege)
Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities na English Activitites.
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kushiriki katika vikundi shuleni kama vile chama cha ukulima kuimba na kukariri mashairi kuhusu ndege wa nyumbani.
Uhusiano na Maadili:
upendo kwa ndege wanaofugwa uwajibikaji katika kutunza ndege.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kutunza ndege na wanyama.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza anavyotumia msamiati wa ndege wanaofugwa katika mawasiliano
- kuchunguza anavyotumia juu ya na chini ya katika mawasiliano
- kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
- kufuatilia mwandiko wake.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anasikiliza na kusimulia hadithi kwa ukakamavu na ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye kwa wepesi na ufasaha
- anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
- anatumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi zenye ubunifu wa hali ya juu
- anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, hati nadhifu na kwa haraka.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anasikiliza na kusimulia hadithi kwa ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye kwa ufasaha
- anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- anatumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi
- anaandika kisa kwa
mtiririko na hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anasikiliza na kusimulia hadithi
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye
- anafahamu baadhi ya hadithi aliyosoma na kusomewa
- ana changamoto katika kutumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi
- anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kusimulia hadithi
- ana changamoto katika kusoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu ndege ampendaye
- ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- ana changamoto katika kutumia juu ya na chini ya kutunga sentensi sahihi
ana changamoto katika kuandika kisa.