MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua msamiati uliotumiwa katika hadithi ili kuwezesha ufahamu,
- kusikiliza hadithi zikisomwa na mwalimu kuhusu sokoni ili kujenga usikivu,
- kusoma hadithi kuhusu sokoni ili kuimarisha stadi ya kusoma,
- kufahamu hadithi aliyoisoma au kusomewa kuhusu sokoni ili kupata ujumbe,
- kuchangamkia kusoma hadithi ili kujenga ari ya kuendeleza ujifunzaji.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
- Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
- Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma hadithi.
- Mwanafunzi ashiriki kusoma darasani, wakiwa wawili na baadaye asome peke yake.
- Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
- Mwanafunzi asikilize mwalimu akisoma hadithi.
- Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ikisomwa kupitia vifaa vya kiteknolojia huku mwanafunzi akikumbushwa kusikiliza kwa makini.
- Wanafunzi waweza kusomeana hadithi wakiwa wawili wawili au katika vikundi.
- Wanafunzi waweza kushirikishwa kupanga upya sentensi zilizoparaganywa zinazohusu sokoni katika vikundi.
- Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kwa kutumia jitabu lililowekwa mbele ya darasa
- Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyoisoma.
- Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kutokana na hadithi.
MASWALI DADISI
- Ni watu wepi wametajwa katika hadithi?
- Ni vitu gani vimetajwa katika hadithi?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza hamu ya kuendeleza ujifunzaji – kusoma hadithi.
Uhusiano na masuala mtambuko:
elimu ya maendeleo endelevu: elimu ya masuala ya kifedha – kujadili umuhimu wa sokoni.
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji: kushiriki katika kuigiza shughuli za sokoni.
Uhusiano na Maadili:
uadilifu katika shughuli za sokoni umoja – Hamna biashara inayoweza kunawiri pasipo na umoja heshima ni muhimu popote watu wanapoingiliana hasa sokoni uwajibikaji – Mwenye biashara na mnunuzi sharti wawajibike katika shughuli husika.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kusaidia jamii katika shughuli zinazohusu soko.
Mapendekezo ya Tathmini:
• kuchunguza anavyotumia msamiati wa sokoni katika mawasiliano
- kuchunguza anavyotumia ndani ya na nje ya katika mawasiliano
- kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
- kufuatilia mwandiko wake.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua na kutumia msamiati unaotumika sokoni
- anasimulia visa kuhusu sokoni kwa ubunifu na ukakamavu
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu sokoni kwa ufasaha
- anatumia ndani ya na nje ya kutunga sentensi sahihi zenye ubunifu wa hali ya juu
- anaandika kisa kinachohusiana na sokoni kwa ubunifu, mtiririko, hati nadhifu na kwa kasi ifaayo.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua msamiati unaotumika sokoni
- anasimulia visa kuhusu sokoni kwa ukakamavu
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu sokoni
- anatumia ndani ya na nje ya kutunga sentensi sahihi
- anaandika kisa kinachohusiana na sokoni kwa mtiririko na hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua baadhi ya msamiati unaotumika sokoni
- anasimulia baadhi ya visa kuhusu sokoni
- anasoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu sokoni
- ana changamoto kiasi katika kutumia ndani ya na nje ya kutunga sentensi sahihi
- anaandika kisa kinachohusiana na sokoni kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutambua msamiati unaotumika sokoni
- ana changamoto katika kusimulia visa kuhusu sokoni
- ana changamoto katika kusoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu sokoni
- ana changamoto katika kutumia ndani ya na nje ya kutunga sentensi sahihi
- ana changamoto katika kuandika kisa kinachohusiana na sokoni.