MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutamka sauti nne za herufi moja katika kuimarisha mazungumzo,
- kutambua sauti za herufi moja zilizofunzwa katika maneno ili kuimarisha mazungumzo,
- kutambua majina ya herufi zinazowakilisha sauti lengwa katika kuimarisha stadi ya kusoma,
- kusoma herufi za sauti moja katika kujenga stadi ya kusoma,
- kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa katika kujenga stadi ya kusoma,
- kusoma vifungu vilivyo na maneno yaliyo na sauti lengwa ili kujenga stadi ya kusoma,
- kuandika maumbo ya herufi zinazowakilisha sauti lengwa katika kuimarisha stadi ya kuandika,
- h) kuchangamkia kutumia maneno yanayojumuisha sauti zilizofunzwa katika mawasiliano ya kila siku.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi atambue sauti /w/, /e/, /i/ na /h/ katika maneno.
- Mwanafunzi amsikilize mwalimu akitamka sauti lengwa, kisha atamke pamoja na mwalimu na mwishowe atamke akiwa peke yake, wawili wawili na kama darasa.
- Mwanafunzi atumie teknolojia (papaya) kusikiliza matamshi ya sauti lengwa.
- Mwanafunzi atambue herufi zinazowakilisha sauti lengwa kwa kutumia kadi za herufi. Mwanafunzi aambatanishe silabi kusoma maneno yanayotokana na sauti lengwa. Mwanafunzi atenganishe silabi katika kutambua sehemu mbalimbali za maneno. Wanafunzi waweza kusikiliza mgeni mwalikwa mwenye umahiri wa kutamka sauti lengwa.
- Mwanafunzi afinyange maumbo ya herufi za sauti lengwa.
- Mwanafunzi aandike maumbo ya herufi za sauti alizosoma hewani na vitabuni.
- Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi na kuchanganua yaliyo marefu zaidi.
- Wanafunzi waweza kusoma hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa kama darasa au wawili wawili.
- Mwanafunzi aweza kusikiliza na kusoma hadithi kupitia vifaa vya kiteknolojia kama vile tarakilishi, projekta n.k.
- Mwanafunzi aandike imla ya maneno yaliyo na herufi za sauti alizofunzwa na kuyaandika.
MASWALI DADISI
- Ni sauti zipi unazojua kutamka?
- Unajua kusoma herufi na maneno yapi?
- Unajua kuandika herufi na maneno yapi?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – mwanafunzi anashiriki katika makundi kuimba na kukariri mashairi, kusimulia na kujadiliana hamu ya ujifunzaji: mwanafunzi atajenga msingi wa kusoma na kutafiti zaidi kuhusu usafi ujuzi wa kidijitali : vifaa vya kiteknolojia vinatumiwa katika kusimulia, kuimba na kukariri mashairi ubunifu: mwanafunzi anajenga ubunifu wake anaposimulia na kutunga sentensi akitumia maneno ya vitendo.
Uhusiano na masuala mtambuko: elimu ya afya – usafi wa kibinafsi wanapozingatia usafi wa mwili wao.
Uhusiano na Masomo mengine:
English Activities, Environmental Activities, Health and Nutrition na Religious Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kazi ya vikundi shughuli za vikundi vya ushirika shuleni michezo nyimbo na mashairi kuhusu usafi wa mwili.
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:
kusisitiza kuhusu utunzaji wa mwili miongoni mwa wenzake kulinda usiri wa mwili wake.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuuliza maswali kuhusu jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili,
- kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa,
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa,
- kuchunguza jinsi anavyotumia huyu na hawa katika sentensi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
lKuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
- anaelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili kwa ufasaha
- anatumia msamiati wa usafi wa mwili kwa ubunifu katika sentensi
- anasoma kwa ufasaha
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
- anatumia huyu na hawa kutunga sentensi kwa ubunifu
- anaandika kwa hati nadhifu.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa vyema
- anaelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili
- anatumia msamiati unaotumika katika usafi wa mwili ifaavyo katika sentensi.
- anasoma ifaavyo
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- anatumia huyu na hawa kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
- anaelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili
- ana changamoto katika kutumia baadhi ya misamiati ya usafi wa mwili ifaavyo katika sentensi
- anasoma baadhi ya kazi anazopewa
- anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto za kutumia umoja na wingi wa majina lengwa katika kutunga sentensi
- anaandika kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti lengwa vyema
- ana changamoto katika kuelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili
- ana changamoto katika kutumia msamiati usafi wa mwili ifaavyo katika sentensi
- ana changamoto katika kusoma
- Ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia umoja na wingi wa majina lengwa katika kutunga sentensi
- ana changamoto katika kuandika.