MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua majina ya sehemu za mwili za nje katika umoja na wingi ili kuimarisha mawasiliano,
- kutumia majina ya sehemu za mwili za nje kwenye sentensi katika umoja na wingi ili kuimarisha mawasiliano,
- kusoma sentensi zinazojumuisha sehemu za mwili za nje katika umoja na wingi ili kuimarisha stadi ya kusoma,
- kuandika sentensi zinazojumuisha sehemu za mwili za nje katika umoja na wingi ili kuimarisha stadi ya kuandika,
- kufurahia kurejelea sehemu za mwili za nje katika umoja na wingi katika mawasiliano.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi atunge sentensi kwa kurejelea sehemu za mwili za nje katika umoja na wingi.
- Mwanafunzi asome sentensi zinazorejelea sehemu za mwili za nje katika umoja na wingi.
- Mwanafunzi aandike sentensi zinazorejelea sehemu za mwili za nje katika umoja na wingi.
- Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia majina ya sehemu za mwili za nje katika umoja na wingi.
- Mwanafunzi aweza kunakili sentensi katika umoja na wingi.
- Wanafunzi watunge sentensi katika umoja na wingi kwa vikundi.
MASWALI DADISI
- Je, ni sehemu gani za mwili unazoweza kutaja katika umoja na wingi?
- Je, waweza kutumia majina gani ya sehemu za mwili za nje katika sentensi?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – kupanga kujadiliana umuhimu wa sehemu za mwili; Kufanya kazi kwa vikundi hamu ya ujifunzaji: hamu ya kutaka kujua vitu vingine katika umoja na wingi ujuzi wa kidijitali: kuna mapendekezo ya kutumia vifaa vya kiteknolojia kufunzia ubunifu: utunzi wa sentensi katika umoja na wingi.
Uhusiano na masuala mtambuko na Maadili:
stadi za maisha – kujitambua na kujithamini anapotaja sehemu zake za mwili; kujionea fahari kwa maumbile yake uraia: utangamano wa kijamii – kushirikiana katika vikundi.
Uhusiano na Masomo mengine:
English Activities, Environmental Activities na Religious Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kazi ya vikundi shughuli za vikundi vya ushirika shuleni michezo nyimbo na mashairi.
Uhusiano na maadili: Uwajibikaji mapenzi kwa mwili wake.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:
kusisitiza kuhusu utunzaji wa mwili miongoni mwa wenzake kulinda usiri wa mwili wake.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza jinsi anavyotambua sehemu mbalimbali za mwili
- kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa
- kuchunguza jinsi anavyotumia umoja na wingi wa majina katika sentensi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa ifaavyo na kwa ukakamavu
- anaelezea sehemu lengwa za mwili ifaavyo
- anatumia majina ya sehemu lengwa za mwili kwa ubunifu katika sentensi
- anasoma kwa ufasaha
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
- anatumia umoja na wingi wa majina lengwa katika kutunga sentensi ifaavyo kila wakati
- anaandika kwa hati nadhifu na kwa haraka.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa vyema
- anataja sehemu lengwa za mwili ifaavyo
- anatumia majina ya sehemu lengwa za mwili ifaavyo katika sentensi
- anasoma ifaavyo
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- anatumia umoja na wingi wa majina lengwa katika kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa
- anataja sehemu lengwa za mwili
- ana changamoto katika kutumia baadhi ya majina ya sehemu lengwa za mwili ifaavyo katika sentensi
- anasoma baadhi ya kazi anazopewa
- anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia umoja na wingi wa baadhi ya majina lengwa kutunga sentensi anaandika kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti lengwa
- ana changamoto katika kutaja baadhi ya sehemu lengwa za mwili
- ana changamoto katika kusoma
- ana changamoto katika kutumia majina ya sehemu lengwa za mwili ifaavyo katika sentensi
- ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu katikahadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia umoja na wingi wa majina lengwa kutunga sentensi
- ana changamoto katika kuandika.