Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua sehemu za mwili zinazopaswa kuangaziwa zaidi katika usafi katika kuimarisha mazungumzo,
  2. kusikiliza hadithi kuhusu usafi wa mwili katika kurejelea stadi ya kusikiliza,
  3. kufahamu masimulizi aliyoyasikiliza katika kurejelea stadi ya kusikiliza,
  4. kusimulia visa vinavyohusu usafi katika kurejelea stadi ya kuzungumza,
  5. kufurahia masimulizi kuhusu usafi kila wakati katika mawasiliano.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

  • Mwanafunzi asimuliwe hadithi kuhusu usafi kisha ashiriki katika mjadala kuhusu usafi wa mwili.
  • Wanafunzi wasimuliane visa kuhusu usafi.
  • Wanafunzi wajadiliane kuhusu sehemu za mwili zinazopaswa kuangaziwa zaidi katika usafi.
  • Wanafunzi wajadiliana kuhusu umuhimu wa usafi maishani.
  • Mwanafunzi aweza kusikiliza mgeni mwalikwa

k.m daktari au nesi akizungumzia juu ya usafi.

  • Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali ya hadithi na maelezo aliyosikia kuhusu usafi.
  • Mwanafunzi aweza kuhusishwa katika kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu usafi wakiigiza vitendo vya usafi.
  • Mwanafunzi aweza kusikiliza nyimbo na mashairi yaliyorekodiwa kwenye vifaa vya kiteknolojia.

MASWALI DADISI

1) Je, ni sehemu zipi za mwili zinazopaswa

kuangaziwa zaidi katika usafi?

  • Je, usafi una umuhimu gani?
  • Je, unaweza kusimulia kisa kuhusu usafi?

 Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:

mawasiliano na ushirikiano –  mwanafunzi anashiriki katika makundi kuimba na kukariri mashairi, kusimulia na kujadiliana  hamu ya ujifunzaji: mwanafunzi atajenga msingi wa kusoma na kutafiti zaidi kuhusu usafi ujuzi wa kidijitali : vifaa vya kiteknolojia vinatumiwa katika kusimulia, kuimba na kukariri mashairi ubunifu: mwanafunzi anajenga ubunifu wake anaposimulia na kutunga sentensi akitumia maneno ya vitendo.

Uhusiano na masuala mtambuko:  elimu ya afya –  usafi wa kibinafsi wanapozingatia usafi wa mwili wao.

Uhusiano na Masomo mengine:  

English Activities, Environmental Activities, Health and Nutrition na Religious Activities  

 Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kazi ya vikundi  shughuli za vikundi vya ushirika shuleni michezo nyimbo na mashairi kuhusu usafi wa mwili.

 Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji.  

Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: 

kusisitiza kuhusu utunzaji wa mwili miongoni mwa wenzake kulinda usiri wa mwili wake.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuuliza maswali kuhusu jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili, 
  • kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa, 
  • kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa, 
  • kuchunguza jinsi anavyotumia huyu na hawa katika sentensi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

lKuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
  • anaelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili kwa ufasaha
  • anatumia msamiati wa usafi wa mwili kwa ubunifu katika sentensi
  • anasoma kwa ufasaha
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi 
  • anatumia huyu na hawa kutunga sentensi kwa ubunifu
  • anaandika kwa hati nadhifu.

Kufikia Matarajio

            Mwanafunzi,

  • anatamka sauti lengwa vyema
  • anaelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili
  • anatumia msamiati unaotumika katika usafi wa mwili ifaavyo katika sentensi.
  • anasoma ifaavyo
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
  • anatumia huyu na hawa kutunga sentensi ifaavyo
  • anaandika kwa hati bora.

         Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
  • anaelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili
  • ana changamoto katika kutumia baadhi ya misamiati ya usafi wa mwili ifaavyo katika sentensi
  • anasoma baadhi ya kazi anazopewa
  • anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika  hadithi na masimulizi kwa usahihi
  • ana changamoto za kutumia umoja na wingi wa majina lengwa katika kutunga sentensi 
  • anaandika kwa hati zinazosomeka.

Mbali na Matarajio

                Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka sauti lengwa vyema
  • ana changamoto katika kuelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili
  • ana changamoto katika kutumia msamiati usafi wa mwili ifaavyo katika sentensi
  • ana changamoto katika kusoma
  • Ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi 
  • ana changamoto katika kutumia umoja na wingi wa majina lengwa katika kutunga sentensi
  • ana changamoto katika  kuandika.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *