MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua msamiati uliotumiwa katika hadithi ili kuimarisha mawasiliano,
- kusikiliza hadithi zikisomwa na mwalimu zinazohusu usafi wa mwili katika kujenga stadi ya kusoma,
- kusoma hadithi zinazohusu usafi wa mwili katika kujenga stadi ya kusoma,
- kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa kuhusu usafi wa mwili ili kuimarisha mawasiliano,
- kudumisha usafi katika maisha ya kila siku.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
- Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
- Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma na kusomewa hadithi.
- Mwanafunzi asome hadithi baada ya mwalimu, kisha pamoja na mwalimu na baadaye akiwa peke yake au wawili wawili.
- Mwanafunzi aeleze maana na matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
- Mwanafunzi asikilize mwalimu anaposoma hadithi, asome pamoja na mwalimu kisha asome peke yake.
- Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ya mwalimu au hadithi iliyorekodiwa kuhusu usafi.
- Wanafunzi waweza kusomeana hadithi wakiwa wawili wawili na katika vikundi.
- Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kupitia vifaa vya kiteknolojia kama vile tarakilishi, projekta n.k.
- Mwanafunzi asome maneno yanayohusu usafi kwenye kadi.
- Mwanafunzi aweza kuhusishwa katika kuigiza vitendo vinavyohusu usafi wa mwili.
- Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kwa kutumia jitabu lililowekwa mbele ya darasa.
- Mwanafunzi aweza kuonyeshwa picha zinazoashiria vitendo vya usafi wa mwili.
- Mwanafunzi aulize na kujibu maswali kutokana na hadithi.
MASWALI DADISI
- Je, ni nini maana ya usafi gani?
- Je, ni matayarisho yapi unayofanya kabla ya kuja shuleni?
- Unafikiri ni nini kitakachotokea katika hadithi hii?
- Je, ni hadithi gani
umewahi kusoma?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – mwanafunzi anashiriki katika makundi kuimba na kukariri mashairi, kusimulia na kujadiliana hamu ya ujifunzaji: mwanafunzi atajenga msingi wa kusoma na kutafiti zaidi kuhusu usafi ujuzi wa kidijitali : vifaa vya kiteknolojia vinatumiwa katika kusimulia, kuimba na kukariri mashairi ubunifu: mwanafunzi anajenga ubunifu wake anaposimulia na kutunga sentensi akitumia maneno ya vitendo.
Uhusiano na masuala mtambuko: elimu ya afya – usafi wa kibinafsi wanapozingatia usafi wa mwili wao.
Uhusiano na Masomo mengine:
English Activities, Environmental Activities, Health and Nutrition na Religious Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kazi ya vikundi shughuli za vikundi vya ushirika shuleni michezo nyimbo na mashairi kuhusu usafi wa mwili.
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:
kusisitiza kuhusu utunzaji wa mwili miongoni mwa wenzake kulinda usiri wa mwili wake.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuuliza maswali kuhusu jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili,
- kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa,
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa,
- kuchunguza jinsi anavyotumia huyu na hawa katika sentensi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
lKuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
- anaelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili kwa ufasaha
- anatumia msamiati wa usafi wa mwili kwa ubunifu katika sentensi
- anasoma kwa ufasaha
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
- anatumia huyu na hawa kutunga sentensi kwa ubunifu
- anaandika kwa hati nadhifu.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa vyema
- anaelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili
- anatumia msamiati unaotumika katika usafi wa mwili ifaavyo katika sentensi.
- anasoma ifaavyo
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- anatumia huyu na hawa kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
- anaelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili
- ana changamoto katika kutumia baadhi ya misamiati ya usafi wa mwili ifaavyo katika sentensi
- anasoma baadhi ya kazi anazopewa
- anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto za kutumia umoja na wingi wa majina lengwa katika kutunga sentensi
- anaandika kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti lengwa vyema
- ana changamoto katika kuelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili
- ana changamoto katika kutumia msamiati usafi wa mwili ifaavyo katika sentensi
- ana changamoto katika kusoma
- Ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia umoja na wingi wa majina lengwa katika kutunga sentensi
- ana changamoto katika kuandika.