MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua matumizi ya huyu na hawa katika mawasiliano,
- kusoma sentensi zinazojumuisha huyu na hawa ili kuimarisha mawasiliano,
- kutumia huyu na hawa katika sentensi ili kuimarisha mawasiliano,
- kuandika sentensi kwa kutumia huyu na hawa katika kuimarisha stadi ya kuandika,
- kuthamini utunzi wa sentensi sanifu katika mawasiliano.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi atunge sentensi zenye matumizi ya huyu na hawa k.m. Huyu anakata kucha – Hawa wanakata kucha; Huyu anachana nywele – Hawa wanachana nywele.
- Mwanafunzi aandike sentensi zinazojumuisha matumizi ya huyu na hawa.
- Mwanafunzi asome sentensi zinazojumuisha matumizi ya huyu na hawa.
- Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia huyu na hawa.
- Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwenye tarakilishi kupitia mchezo wa kuburura na kutia kapuni.
MASWALI DADISI
- Je, unajua ni kwa nini tunatumia huyu na hawa?
- Je, utatumia neno lipi kuonyesha kwamba mtu ni mmoja?
- Watu wakiwa wengi unaonyesha vipi?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – mwanafunzi anashiriki katika makundi kuimba na kukariri mashairi, kusimulia na kujadiliana hamu ya ujifunzaji: mwanafunzi atajenga msingi wa kusoma na kutafiti zaidi kuhusu usafi ujuzi wa kidijitali : vifaa vya kiteknolojia vinatumiwa katika kusimulia, kuimba na kukariri mashairi ubunifu: mwanafunzi anajenga ubunifu wake anaposimulia na kutunga sentensi akitumia maneno ya vitendo.
Uhusiano na masuala mtambuko: elimu ya afya – usafi wa kibinafsi wanapozingatia usafi wa mwili wao.
Uhusiano na Masomo mengine:
English Activities, Environmental Activities, Health and Nutrition na Religious Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kazi ya vikundi shughuli za vikundi vya ushirika shuleni michezo nyimbo na mashairi kuhusu usafi wa mwili.
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:
kusisitiza kuhusu utunzaji wa mwili miongoni mwa wenzake kulinda usiri wa mwili wake.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuuliza maswali kuhusu jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili,
- kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa,
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa,
- kuchunguza jinsi anavyotumia huyu na hawa katika sentensi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
lKuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
- anaelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili kwa ufasaha
- anatumia msamiati wa usafi wa mwili kwa ubunifu katika sentensi
- anasoma kwa ufasaha
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
- anatumia huyu na hawa kutunga sentensi kwa ubunifu
- anaandika kwa hati nadhifu.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa vyema
- anaelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili
- anatumia msamiati unaotumika katika usafi wa mwili ifaavyo katika sentensi.
- anasoma ifaavyo
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- anatumia huyu na hawa kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
- anaelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili
- ana changamoto katika kutumia baadhi ya misamiati ya usafi wa mwili ifaavyo katika sentensi
- anasoma baadhi ya kazi anazopewa
- anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto za kutumia umoja na wingi wa majina lengwa katika kutunga sentensi
- anaandika kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti lengwa vyema
- ana changamoto katika kuelezea jinsi ya kuzingatia usafi wa mwili
- ana changamoto katika kutumia msamiati usafi wa mwili ifaavyo katika sentensi
- ana changamoto katika kusoma
- Ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia umoja na wingi wa majina lengwa katika kutunga sentensi
- ana changamoto katika kuandika.