MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutamka sauti nne za herufi moja katika kuimarisha stadi ya kuzungumza,
- kutambua sauti za herufi moja zilizofunzwa katika maneno
katika kuimarisha stadi ya kuzungumza,
- kutambua majina ya herufi zinazowakilisha sauti lengwa katika kuimarisha stadi ya kusoma,
- kusoma herufi za sauti moja katika kuimarisha stadi ya kusoma,
- kusoma maneno kwa kutumia
silabi zinazotokana na sautilengwa katika kuimarisha stadi ya kusoma,
- kusoma vifungu vilivyo na maneno yaliyo na sauti lengwa katika kuimarisha stadi ya kusoma,
- kuandika maumbo ya herufi yanayowakilisha sauti lengwa katika kuimarisha stadi ya kusoma,
- kuchangamkia kutumia maneno yanayojumuisha sauti lengwa katika mawasiliano ya kila siku.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi atambue sauti lengwa /s/, /b/, /y/ na /z/ katika maneno.
- Mwanafunzi asikilize mwalimu akitamka sauti lengwa, kisha atamke pamoja na mwalimu na mwishowe atamke akiwa peke yake, wawili wawili na kama darasa.
- Mwanafunzi atumie teknolojia (papaya) kutamkia sauti.
- Mwanafunzi atambue herufi zinazowakilisha sauti lengwa kwa kutumia kadi za herufi.
- Mwanafunzi aambatanishe silabi kusoma maneno yanayotokana na sauti lengwa.
- Mwanafunzi atenganishe silabi katika kutambua sehemu mbalimbali za maneno.
- Wanafunzi waweza kushirikishwa kusikiliza mgeni mwalikwa mwenye umahiri wa kutamka sauti lengwa.
- Mwanafunzi aweza kufinyanga maumbo ya herufi inayowakilisha sauti iliyofunzwa.
- Mwanafunzi aandike maumbo ya herufi za sauti alizosoma hewani na vitabuni.
- Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi au kwa kugawa maneno marefu katika sehemu ndogo ndogo ili kuyasoma kwa urahisi.
- Wanafunzi wasome hadithi zilizo na maneno yanayobeba sauti lengwa kama darasa au wawili wawili.
- Mwanafunzi anaweza kushirikishwa kusikiliza na kusoma hadithi kupitia vifaa vya kiteknolojia kama vile tarakilishi, projekta n.k.
- Mwanafunzi ashirikishwe katika kuandika imla ya maneno yaliyo na herufi za sauti alizofunzwa na kuyaandika.
MASWALI DADISI
- Ni sauti zipi unazoweza kutamka?
- Unajua kusoma herufi na maneno yapi?
- Unajua kuandika herufi na maneno?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
- mawasiliano na ushirikiano – kujadili katika makundi au wawili wawili
• hamu ya ujifunzaji: mwanafunzi atajenga msingi wa kujua vyakula zaidi
- ujuzi wa kidijitali –matumizi ya vifaa vya kiteknolojia.
Uhusiano na masuala mtambuko:
elimu ya afya: magonjwa yanayohusiana na vyakula – kuthamini vyakula vya kiasili.
Uhusiano na Masomo mengine:
Health and Nutrition Activities na Environmental Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
- kazi ya vikundi
- michezo
- nyimbo na Mashairi kuhusu vyakula vya kiasili.
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:
kuwahamasisha wengine katika jamii kuhusu umuhimu wa vyakula vya kiasili.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuuliza maswali kuhusu vyakula vya kiasili
- kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa
- kuchunguza jinsi anavyotumia –angu na -etu katika sentensi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
- anaelezea mifano ya vyakula vya
kiasili
- anatumia msamiati wa vyakula vya kiasili kwa ubunifu katika sentensi
- anasoma kwa ufasaha
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
- anatumia -angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati nadhifu.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa vyema
- anataja mifano ya vyakula vya
kiasili
- anatumia msamiati wa vyakula vya kiasili ifaavyo katika sentensi
- anasoma ifaavyo
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- anatumia -angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati bora.
. Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
- anataja mifano ya vyakula vya
kiasili
- ana changamoto katika kutumia baadhi ya msamiati wa vyakula vya kiasili katika sentensi
- anasoma baadhi ya kazi anazopewa
- anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia -angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
- ana changamoto katika kusoma.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti lengwa vyema
- ana changamoto katika kutaja mifano ya vyakula vya kiasili
- ana changamoto katika kutumia msamiati wa vyakula vya kiasili katika sentensi
- ana changamoto katika kusoma
- ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi
- ana changamoto katika kutumia angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
- ana changamoto katika kuandika.