Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua vyakula vya kiasili ili kuimarisha lishe bora,
  2. kusoma majina ya vyakula mbalimbali ili kuimarisha stadi ya kusoma,
  3. kuandika majina ya vyakula katika kuimarisha stadi ya kuandika,
  4. kutumia majina ya vyakula katika sentensi sahihi,
  5. kuthamini vyakula vya kiasili katika maisha ya kila siku.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

  • Mwanafunzi atambue vyakula mbalimbali vya kiasili kwa kutumia vyakula halisi, picha na michoro ya vyakula kama vile mihogo, viazi, mahindi, maharagwe, mboga na matunda.
  • Mwanafunzi atumie msamiati aliyofunzwa kutunga sentensi.
  • Mwanafunzi aandike maneno aliyofunzwa. 
  • Mwanafunzi aweza kupewa kadi za majina ya vyakula vya kiasili asome kwa sauti.
  • Wanafunzi waweza  kuambatanisha majina ya vyakula halisi au michoro na majina yavyo.
  • Wanafunzi waweza kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu vyakula vya kiasili.
  • Wanafunzi waweza kuandika majina ya vyakula wanavyovijua katika vikundi.
  • Wanafunzi waweza kutazama picha za vyakula mbalimbali kupitia kwa vifaa vya kiteknolojia.

MASWALI DADISI

  1. je, ni vyakula vipi vya kiasili unavyopenda ? 
  2. Vyakula vipi hukuzwa shambani?

 Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:

  • mawasiliano na ushirikiano –  kujadili katika makundi au wawili wawili •             hamu ya ujifunzaji: mwanafunzi atajenga msingi wa kujua vyakula zaidi
  • ujuzi wa kidijitali –matumizi ya vifaa vya kiteknolojia.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

elimu ya afya: magonjwa yanayohusiana na vyakula  – kuthamini vyakula vya kiasili.

Uhusiano na Masomo mengine:  

Health and Nutrition Activities na Environmental Activities

 Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

  • kazi ya vikundi 
  • michezo
  • nyimbo na Mashairi kuhusu vyakula vya kiasili.

Uhusiano na Maadili:  

uwajibikaji

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: 

kuwahamasisha wengine katika jamii kuhusu umuhimu wa vyakula vya kiasili.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuuliza maswali kuhusu vyakula vya kiasili 
  • kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa 
  • kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa 
  • kuchunguza jinsi anavyotumia –angu na -etu katika sentensi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
  • anaelezea mifano ya vyakula vya

kiasili

  • anatumia msamiati wa  vyakula vya kiasili kwa ubunifu katika sentensi
  • anasoma kwa ufasaha
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi 
  • anatumia -angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
  • anaandika kwa hati nadhifu.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti lengwa vyema
  • anataja mifano ya vyakula vya

kiasili 

  • anatumia msamiati wa vyakula vya kiasili ifaavyo katika sentensi
  • anasoma ifaavyo
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi 
  • anatumia -angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
  • anaandika kwa hati bora.

 .  Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
  • anataja mifano ya vyakula vya

kiasili

  • ana changamoto katika kutumia baadhi ya msamiati wa  vyakula vya kiasili katika sentensi
  • anasoma baadhi ya kazi anazopewa
  • anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi 
  • ana changamoto katika kutumia -angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
  • ana changamoto katika kusoma. 

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka sauti lengwa vyema
  • ana changamoto katika kutaja mifano ya vyakula vya kiasili 
  • ana changamoto katika kutumia msamiati wa vyakula vya kiasili katika sentensi
  • ana changamoto katika kusoma
  • ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi

ana changamoto katika kutumia angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *