MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutamka sauti nne za herufi moja katika kuimarisha mazungumzo,
- kutambua sauti za herufi moja zilizofunzwa katika maneno,
- kutambua majina ya herufi zinazowakilisha sauti lengwa katika kuimarisha stadi ya kusoma,
- kusoma herufi za sauti moja katika kujenga stadi ya kusoma,
- kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa katika kujenga stadi ya kusoma,
- kusoma vifungu vilivyo na maneno yaliyo na sauti lengwa ili kujenga stadi ya kusoma,
- kuandika maumbo ya herufi zinazowakilisha sauti lengwa katika kuimarisha stadi ya kuandika,
- kuchangamkia kutumia maneno yanayojumuisha sauti zilizofunzwa katika mawasiliano ya kila siku.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi atambue sauti /t/, /l/, /n/ na /o/ katika maneno.
- Mwanafunzi asikilize mwalimu anapotamka sauti lengwa, kisha atamke pamoja na mwalimu na mwishowe atamke akiwa peke yake, wawili wawili au kama darasa.
- Mwanafunzi atumie teknolojia (papaya) kutamkia sauti.
- Mwanafunzi atambue herufi inayowakilisha sauti lengwa kwa kutumia kadi za herufi.
- Mwanafunzi aambatanishe silabi kusoma maneno yanayotokana na sauti lengwa.
- Mwanafunzi atenganishe silabi katika kutambua sehemu mbalimbali za maneno.
- Wanafunzi waweza kushirikishwa kusikiliza mgeni mwalikwa mwenye umahiri wa kutamka sauti lengwa.
- Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi na kuchanganua yaliyo marefu zaidi.
- Wanafunzi wasome hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa kama darasa au wawili wawili.
- Mwanafunzi asikilize na kusoma hadithi kupitia vifaa vya kiteknolojia kama vile tarakilishi, projekta n.k.
- Mwanafunzi afinyange na aandike maumbo ya herufi za sauti alizosoma hewani na vitabuni.
- Mwanafunzi aandike maneno yaliyo na herufi za sauti alizofunzwa kwa kunakili aliyoandika mwalimu.
MASWALI DADISI
- Ni sauti zipi unazojua kutamka?
- Unajua kusoma herufi na maneno yapi?
- Unajua kuandika herufi na maneno yapi?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – kupanga kujadiliana umuhimu wa sehemu za mwili; Kufanya kazi kwa vikundi hamu ya ujifunzaji: hamu ya kutaka kujua vitu vingine katika umoja na wingi ujuzi wa kidijitali: kuna mapendekezo ya kutumia vifaa vya kiteknolojia kufunzia ubunifu: utunzi wa sentensi katika umoja na wingi.
Uhusiano na masuala mtambuko na Maadili:
stadi za maisha – kujitambua na kujithamini anapotaja sehemu zake za mwili; kujionea fahari kwa maumbile yake uraia: utangamano wa kijamii – kushirikiana katika vikundi.
Uhusiano na Masomo mengine:
English Activities, Environmental Activities na Religious Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kazi ya vikundi shughuli za vikundi vya ushirika shuleni michezo nyimbo na mashairi.
Uhusiano na maadili: Uwajibikaji mapenzi kwa mwili wake.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:
kusisitiza kuhusu utunzaji wa mwili miongoni mwa wenzake kulinda usiri wa mwili wake.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza jinsi anavyotambua sehemu mbalimbali za mwili
- kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa
- kuchunguza jinsi anavyotumia umoja na wingi wa majina katika sentensi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa ifaavyo na kwa ukakamavu
- anaelezea sehemu lengwa za mwili ifaavyo
- anatumia majina ya sehemu lengwa za mwili kwa ubunifu katika sentensi
- anasoma kwa ufasaha
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
- anatumia umoja na wingi wa majina lengwa katika kutunga sentensi ifaavyo kila wakati
- anaandika kwa hati nadhifu na kwa haraka.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa vyema
- anataja sehemu lengwa za mwili ifaavyo
- anatumia majina ya sehemu lengwa za mwili ifaavyo katika sentensi
- anasoma ifaavyo
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- anatumia umoja na wingi wa majina lengwa katika kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa
- anataja sehemu lengwa za mwili
- ana changamoto katika kutumia baadhi ya majina ya sehemu lengwa za mwili ifaavyo katika sentensi
- anasoma baadhi ya kazi anazopewa
- anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia umoja na wingi wa baadhi ya majina lengwa kutunga sentensi anaandika kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti lengwa
- ana changamoto katika kutaja baadhi ya sehemu lengwa za mwili
- ana changamoto katika kusoma
- ana changamoto katika kutumia majina ya sehemu lengwa za mwili ifaavyo katika sentensi
- ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu katikahadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia umoja na wingi wa majina lengwa kutunga sentensi
- ana changamoto katika kuandika.