MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua msamiati unaohusiana na shughuli za shambani ili kuimarisha mawasiliano,
- kusoma maneno na sentensi kuhusu shambani ili kuimarisha usomaji,
- kutunga sentensi akitumia msamiati wa shambani ili kuimarisha mawasiliano,
- kuandika maneno na sentensi zinazojumuisha msamiati wa shambani katika kujenga uandishi bora,
- kuthamini matumizi ya msamiati wa shambani katika mawasiliano.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi asome msamiati wa shambani kama vile jembe, shoka, upanga, kifyekeo, plau, trekta, lima, fyeka, panda na kwekwe katika kadi na chati.
- Mwanafunzi ataje majina ya vifaa halisi, picha au michoro anavyoonyeshwa.
- Mwanafunzi atazame video ya vifaa vya shambani vikifanya kazi kwenye tarakilishi au tabuleti.
- Mwanafunzi achore maumbo ya vifaa vinavyotumika shambani.
- Wanafunzi waambatanishe kadi za maneno na vifaa halisi au picha wakiwa katika vikundi.
- Wanafunzi waweza kushiriki katika nyimbo na mashairi kuhusu shambani.
- Mwanafunzi aandike majina ya vifaa vinavyotumika shambani.
- Mwanafunzi atunge na kusoma sentensi akitumia msamiati wa shambani.
MASWALI DADISI
- Je, wajua vifaa vipi vinavyotumika shambani?
- Ni kifaa kipi cha shamba unachoweza kuchora?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – Wanatumia lugha faafu darasani. Vilevile wanashirikiana katika kazi ya vikundi. ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.
ubunifu: mwanafunzi napoandika au kusimulia kisa kufikiria kwa kina na kutatua matatizo – mwanafunzi anapojibu maswali ambayo majibu yake hayapatikani moja kwa moja kutoka kwenye kisa hamu ya ujifuzaji – mwanafunzi atapata hamu ya kutaka kujua matumizi ya vifaa vya shambani.
Uhusiano na masuala mtambuko:
elimu ya maendeleo endelevu: athari za majanga – kujua athari za vifaa vya shambani uraia : kuthamini kilimo katika kukuza uchumi wa nchi.
Uhusiano na masomo mengine: Environmental activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kushiriki katika vikundi vya ushirika shuleni vinavyohusu ukulima kushiriki katika kilimo shuleni.
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji katika kutunza vifaa vya shambani kutunza vifaa vya shambani.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika ukulima nyumbani
Kuwahamasisha wengine wa rika lake kuhusu umuhimu wa kilimo.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
- kuchunguza anavyotumia msamiati wa shambani katika mawasiliano
- kuchunguza anavyotumia nafsi ya tatu wakati ujao katika mawasiliano • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kufuatilia mwandiko wake.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
- anasimulia shughuli zinazofanyika shambani kwa ubunifu
- anasoma hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
- anafahamu kwa urahisi hadithi aliyosoma na kusomewa
- anaandika kisa kifupi kwa hati nadhifu na ubunifu
- anatunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi kila wakati.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti ipasavyo
- anasimulia shughuli zinazofanyika shambani
- anasoma hadithi kwa ufasaha.
- anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- anaandika kisa kifupi kwa hati bora
- anatunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka baadhi ya sauti ipasavyo
- anasimulia baadhi ya shughuli za shambani
- anasoma hadithi kwa ufasaha
- ana chamgamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- anajaribu kuandika kisa kwa hati inayosomeka
- ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti alizofunzwa
- ana changamoto katika kusimulia shughuli za shambani
- ana changamoto katika kusoma hadithi
- ana chamgamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- ana changamoto katika kuandika kisa
- ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi