MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kusikiliza kwa makini masimulizi kuhusu shambani katika kujenga usikivu
- kutaja majina ya vifa vinavyotumika shambani ili kuimarisha stadi ya kuzungumza
- kuelezea vifaa vinavyotumika shambani ili kuimarisha stadi ya kuzungumza
- kuelezea shughuli zinazofanyika shambani ili kuimarisha stadi ya kuzungumza
- kutambua matumizi ya vifaa vinavyotumika shambani ili kuimarisha stadi ya kuzungumza
f) kuthamini umuhimu wa vifaa vinavyotumika shambani.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi kusimulie visa kuhusu shambani.
- Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu vifaa vinavyotumika shambani kama vile; jembe, shoka, upanga, kifyekeo, plau, trekta, lima, fyeka na panda akionyeshwa vifaa halisi, picha au michoro.
- Mwanafunzi aelezee umuhimu wa vifaa vinavyotumika shambani.
- Mwanafunzi aweza kushirikishwa katika nyimbo au mashairi kuhusu vifaa vinavyotumika shambani.
- Mwanafunzi aweza kushirikishwa katika kuigiza vitendo vinavyofanywa shambani kama vile kulima, kufyeka na kupanda.
- Mwanafunzi aweza kutazama video inayoonyesha jinsi vifaa mbalimbali vinavyotumika shambani
- Mwanafunzi anaweza kutumia tarakilishi kutambua vifaa mbalimbali kwa majina vilivyo.
MASWALI DADISI
- Je, ni vifaa vipi hutumika shambani?
- Ni shughuli zipi zinazofanyika shambani?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – Wanatumia lugha faafu darasani. Vilevile wanashirikiana katika kazi ya vikundi. ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.
ubunifu: mwanafunzi napoandika au kusimulia kisa kufikiria kwa kina na kutatua matatizo – mwanafunzi anapojibu maswali ambayo majibu yake hayapatikani moja kwa moja kutoka kwenye kisa hamu ya ujifuzaji – mwanafunzi atapata hamu ya kutaka kujua matumizi ya vifaa vya shambani.
Uhusiano na masuala mtambuko:
elimu ya maendeleo endelevu: athari za majanga – kujua athari za vifaa vya shambani uraia : kuthamini kilimo katika kukuza uchumi wa nchi.
Uhusiano na masomo mengine: Environmental activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kushiriki katika vikundi vya ushirika shuleni vinavyohusu ukulima kushiriki katika kilimo shuleni.
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji katika kutunza vifaa vya shambani kutunza vifaa vya shambani.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika ukulima nyumbani
Kuwahamasisha wengine wa rika lake kuhusu umuhimu wa kilimo.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
- kuchunguza anavyotumia msamiati wa shambani katika mawasiliano
- kuchunguza anavyotumia nafsi ya tatu wakati ujao katika mawasiliano • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kufuatilia mwandiko wake.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
- anasimulia shughuli zinazofanyika shambani kwa ubunifu
- anasoma hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
- anafahamu kwa urahisi hadithi aliyosoma na kusomewa
- anaandika kisa kifupi kwa hati nadhifu na ubunifu
- anatunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi kila wakati.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti ipasavyo
- anasimulia shughuli zinazofanyika shambani
- anasoma hadithi kwa ufasaha.
- anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- anaandika kisa kifupi kwa hati bora
- anatunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka baadhi ya sauti ipasavyo
- anasimulia baadhi ya shughuli za shambani
- anasoma hadithi kwa ufasaha
- ana chamgamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- anajaribu kuandika kisa kwa hati inayosomeka
- ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti alizofunzwa
- ana changamoto katika kusimulia shughuli za shambani
- ana changamoto katika kusoma hadithi
- ana chamgamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- ana changamoto katika kuandika kisa
- ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi