Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

a) kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada ili

       kujenga stadi ya uandishi,

 b) kufurahia uandishi wa visa tofauti ili kuimarisha mawasiliano andishi.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

 • Mwanafunzi apewe hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka.
 • Mwanafunzi aelezee yaliyo muhimu katika uandishi

k.v. mwandiko nadhifu, maudhui, mtiririko n.k.

 • Mwanafunzi asome kielelezo cha kisa kilichoandikwa na mwanafunzi au mtu mwingine mwenye umahiri wa kuandika.
 • Wanafunzi waweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili.

• Mwanafunzi aandike kisa kifupi kinachohusiana na mada. Kisa hiki kifuate hatua tano za uandishi:

maandalizi, nakala ya kwanza, marejeleo, uhariri na uchapishaji. 

MASWALI DADISI

 1. Je, ni mambo yapi yanayofaa kuzingatiwa unapoandika kisa?
 2. Je, ni visa gani unavyoweza kuandika juu ya shamba?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – Wanatumia lugha faafu darasani. Vilevile wanashirikiana katika kazi ya vikundi. ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.

ubunifu: mwanafunzi napoandika au kusimulia kisa kufikiria kwa kina na kutatua matatizo – mwanafunzi anapojibu maswali ambayo majibu yake hayapatikani moja kwa moja kutoka kwenye kisa  hamu ya ujifuzaji – mwanafunzi atapata hamu ya kutaka kujua matumizi ya vifaa vya shambani.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

elimu ya maendeleo endelevu: athari za majanga – kujua athari za vifaa vya shambani uraia : kuthamini kilimo katika kukuza uchumi wa nchi.

Uhusiano na masomo mengine: Environmental activities

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kushiriki katika vikundi vya ushirika shuleni vinavyohusu ukulima kushiriki katika kilimo shuleni. 

Uhusiano na Maadili:                                       

uwajibikaji katika kutunza vifaa vya shambani kutunza vifaa vya shambani.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika ukulima nyumbani

Kuwahamasisha wengine wa rika lake kuhusu umuhimu wa kilimo.

Mapendekezo ya Tathmini:

 • kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
 • kuchunguza anavyotumia msamiati wa shambani katika mawasiliano
 • kuchunguza anavyotumia nafsi ya tatu wakati ujao katika mawasiliano • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
 • kufuatilia mwandiko wake.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
 • anasimulia shughuli zinazofanyika shambani kwa ubunifu
 • anasoma hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
 • anafahamu kwa urahisi hadithi aliyosoma na kusomewa
 • anaandika kisa kifupi kwa hati nadhifu na ubunifu
 • anatunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi kila wakati.

Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka sauti ipasavyo
 • anasimulia shughuli zinazofanyika shambani
 • anasoma hadithi kwa ufasaha.
 • anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
 • anaandika kisa kifupi kwa hati bora
 • anatunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi.

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka baadhi ya sauti ipasavyo
 • anasimulia baadhi ya shughuli za shambani
 • anasoma hadithi kwa ufasaha
 • ana chamgamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
 • anajaribu kuandika kisa kwa hati inayosomeka
 • ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi.

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

 • ana changamoto katika kutamka sauti alizofunzwa 
 • ana changamoto katika kusimulia shughuli za shambani
 • ana changamoto katika kusoma hadithi  
 • ana chamgamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
 • ana changamoto katika kuandika kisa
 • ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi

CBC Grade 3-Kiswahili Curriculum Designs -1.0-SHAMBANI-Mada Ndogo-1.6-Sarufi:Nafsi ya tatu,wakati ujao ,umoja na wingi.

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

 1. kutambua maneno na viambishi vinavyotumika kuonyeshanafsi ya tatu na wakati ujao katika umoja na wingi ili kuimarisha mawasiliano,
 2. kutumia nafsi ya tatu wakati ujao hali ya umoja na wingi katika sentensi kwa usahihi ili kuimarisha mawasiliano,
 3. kusoma vifungu vilivyo na nafsi ya tatu, wakati ujao kwa umoja na wingi ili kujenga usomaji,
 4. kuandika vifungu vilivyo na nafsi ya tatu, wakati ujao kwa umoja na wingi ili kujenga uandishi bora,
 5. kufurahia kutumia nafsi ya tatu wakati ujao hali ya umoja na wingi  katika mawasiliano.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

 • Mwanafunzi atumie nafsi ya tatu wakati ujao hali ya umoja na wingi katika mazungumzo.
 • Mwanafunzi atumie nafsi ya tatu wakati ujao hali ya umoja na wingi katika sentensi.
 • Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia nafsi ya tatu wakati ujao hali ya umoja na wingi.
 • Wanafunzi wanaweza kupewa sentensi zinazojumuisha nafsi na nyakati mbalimbali wazitambue katika vikundi.
 • Mwanafunzi aweza kupewa zoezi katika tarakilishi ili watumie mbinu ya kuburura na kutia kapuni.
 • Mwanafunzi aigize vitendo vya kuashiria nafsi ya kwanza, ya pili na ya tatu huku akitunga sentensi.
 • Mwanafunzi aweza kupata ufafanuzi wa nafsi kwa kutumia vibonzo katika tarakilishi.

MASWALI DADISI

 1. Je, unatumia neno gani kuonyeshea mwenzako akiwa mbali?
 2. Ikiwa nanuia kusafiri kesho, nitasemaje?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – Wanatumia lugha faafu darasani. Vilevile wanashirikiana katika kazi ya vikundi. ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.

ubunifu: mwanafunzi napoandika au kusimulia kisa kufikiria kwa kina na kutatua matatizo – mwanafunzi anapojibu maswali ambayo majibu yake hayapatikani moja kwa moja kutoka kwenye kisa  hamu ya ujifuzaji – mwanafunzi atapata hamu ya kutaka kujua matumizi ya vifaa vya shambani.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

elimu ya maendeleo endelevu: athari za majanga – kujua athari za vifaa vya shambani uraia : kuthamini kilimo katika kukuza uchumi wa nchi.

Uhusiano na masomo mengine: Environmental activities

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kushiriki katika vikundi vya ushirika shuleni vinavyohusu ukulima kushiriki katika kilimo shuleni. 

Uhusiano na Maadili:                                       

uwajibikaji katika kutunza vifaa vya shambani kutunza vifaa vya shambani.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika ukulima nyumbani

Kuwahamasisha wengine wa rika lake kuhusu umuhimu wa kilimo.

Mapendekezo ya Tathmini:

 • kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
 • kuchunguza anavyotumia msamiati wa shambani katika mawasiliano
 • kuchunguza anavyotumia nafsi ya tatu wakati ujao katika mawasiliano • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
 • kufuatilia mwandiko wake.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
 • anasimulia shughuli zinazofanyika shambani kwa ubunifu
 • anasoma hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
 • anafahamu kwa urahisi hadithi aliyosoma na kusomewa
 • anaandika kisa kifupi kwa hati nadhifu na ubunifu
 • anatunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi kila wakati.

Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka sauti ipasavyo
 • anasimulia shughuli zinazofanyika shambani
 • anasoma hadithi kwa ufasaha.
 • anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
 • anaandika kisa kifupi kwa hati bora
 • anatunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi.

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka baadhi ya sauti ipasavyo
 • anasimulia baadhi ya shughuli za shambani
 • anasoma hadithi kwa ufasaha
 • ana chamgamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
 • anajaribu kuandika kisa kwa hati inayosomeka
 • ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi.

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

 • ana changamoto katika kutamka sauti alizofunzwa 
 • ana changamoto katika kusimulia shughuli za shambani
 • ana changamoto katika kusoma hadithi  
 • ana chamgamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
 • ana changamoto katika kuandika kisa
 • ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akizingatia nafsi ya tatu wakati ujao katika umoja na wingi

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *