Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua sauti mbili zinazotamkwa pamoja ili kuimarisha matamshi bora,
  2. kutamka sauti lengwa ili kuimarisha matamshi bora,
  3. kusoma silabi za sauti lengwa ili kuimarisha usomaji,
  4. kuandika silabi zinazotokana na sauti lengwa ili kuimarisha uandishi bora,
  5. kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti

lengwa ili kuimarisha usomaji,

  • kuandika maneno kutokana na silabi zilizofunzwa ili kuimarisha uandishi bora,
  • kusoma hadithi zilizo na maneno yaliyo na sauti lengwa ili kumsaidia mwanafunzi kutamka sauti husika na kuimarisha matamshi na usomaji, 
  • kuchangamkia kutamka sauti lengwa ili kuimarisha mawasiliano.

                 MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

  • Mwanafunzi atambue sauti mw, nd na pw katika maneno.
  • Mwanafunzi asikilize mwalimu akizitamka silabi zinazotokana na sauti lengwa kisha atamke pamoja na mwalimu na baadaye atamke akiwa  pekee, wawili wawili na  darasa zima k.m mwa, mwe, mwi na  mwo. 
  • Mwanafunzi aweza  kutumia teknolojia kama vile papaya, tarakilishi, projekta na kipasasauti kumsaidia kuimarisha matamshi yake.
  • Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akitamka sauti lengwa.
  • Mwanafunzi atambue sauti alizosoma katika maneno kwa mfano k. m mwana, mwananchi, ndoo, ndizi, uzalendo, pwani, pweza na pweke.
  • Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi na kugawa yaliyo marefu zaidi katika sehemu ndogo ndogo.
  • Wanafunzi wasome hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa darasani au wawili wawili. 
  • Mwanafunzi anakili herufi na maneno yanayotokana na sauti alizofunzwa.
  • Mwanafunzi aandike maneno yanayojumuisha sauti lengwa. 
  • Mwanafunzi asikilize imla ya maneno yaliyo na herufi za sauti lengwa na kuyaandika.

MASWALI DADISI

  1. Ni sauti zipi unazojua kutamka?
  2. Unajua kusoma

silabi  zipi katika maneno?

  • Ni herufi na maneno yapi yanayoundwa kutokana na sauti mbili zinazotamkwa pamoja?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

uraia: uzalendo – kushiriki katika kuimba wimbo wa taifa mawasiliano na ushirikiano – kushirikiana pamoja darasani kufikiri kwa kina na kutatua matatizo – Katika kujibu maswali ya ufahamu yasiyo na majibu ya moja kwa moja ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

uraia: uzalendo – kushiriki katika kuimba wimbo wa taifa.

Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities na Movement and Creative Activities.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kushiriki katika uskauti shuleni kupandisha bendera shuleni kushiriki katika kuimba wimbo wa taifa kuimba na kukariri mashairi kuhusu uzalendo. 

Uhusiano na Maadili: 

umoja, uzalendo, haki za kijamii, uwajibikaji, mapenzi kwa nchi, heshima na amani.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika kuimba nyimbo zinazokuza uzalendo katika sherehe mbalimbali.

 Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
  • kuchunguza anavyotumia msamiati wa shambani katika mawasiliano
  • kuchunguza anavyotumia –ake na -ao katika mawasiliano
  • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
  • kufuatilia mwandiko wake
  • kuchunguza anavyotumia lugha katika masimulizi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti ipasavyo na kwa ufasaha
  • anasimulia visa vinavyohusiana na uzalendo kwa ubunifu
  • anasoma hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
  • anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anatunga sentensi sahihi akitumia – ake na -ao kila wakati
  • anaandika kisa kifupi kwa hati nadhifu, ubunifu, mtiririko mwafaka na kwa haraka. 

Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti ipasavyo
  • anasimulia visa vinavyohusiana na uzalendo 
  • anasoma hadithi kwa ufasaha
  • anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anatunga sentensi sahihi akitumia –ake na -ao 
  • anaandika kisa kifupi kwa hati bora na kwa mtiririko ufaao.

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka baadhi ya sauti ipasavyo
  • anasimulia visa vinavyohusiana na uzalendo.
  • anasoma hadithi
  • anafahamu baadhi ya hadithi aliyosoma na kusomewa
  • ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akitumia –ake na -ao 
  • anajaribu kuandika kisa kifupi kwa hati zinazosomeka.

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka  sauti ipasavyo
  • ana changamoto katika kusimulia visa vinavyohusiana na uzalendo
  • ana changamoto katika kusoma hadithi
  • ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
  • ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akitumia –ake na -ao 
  • ana changamoto katika kuandika kisa.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *