MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua msamiati ambao unahusiana na uzalendo ili kuimarisha mawasiliano,
- kusoma msamiati unaohusiana na uzalendo ili kujenga usomaji,
- kueleza maana ya msamiati wa uzalendo ili kuimarisha mawasiliano,
- kutumia msamiati wa uzalendo katika sentensi sahihi ili kuimarisha mawasiliano,
- kuandika maneno yanayohusiana na uzalendo ili kuimarisha uandishi bora,
- kuthamini uzalendo ili kuwa mzalendo kwa nchi yake.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi asome maneno yanayohusiana na uzalendo kama vile; umoja, amani, upendo, bendera, taifa, nchi, raia, gwaride, rangi za bendera kwa kutumia kadi za maneno.
- Mwanafunzi aeleze maana ya msamiati wa uzalendo.
- Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu maana za maneno yanayohusiana na uzalendo
- Mwanafunzi atunge sentensi sahihi kwa kutumia msamiati wa uzalendo.
- Wanafunzi watazame video kuhusu vitendo vya kizalendo k.m. mashujaa wa nchi.
- Mwanafunzi atazame michoro na picha inayolenga maana za maneno kuhusu uzalendo.
- Wanafunzi wajadiliane kuhusu umuhimu wa uzalendo wakiwa kwenye vikundi.
MASWALI DADISI
- Je, uzalendo ni nini?
- Unajua maneno yapi yanayohusiana na uzalendo?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
uraia: uzalendo – kushiriki katika kuimba wimbo wa taifa mawasiliano na ushirikiano – kushirikiana pamoja darasani kufikiri kwa kina na kutatua matatizo – Katika kujibu maswali ya ufahamu yasiyo na majibu ya moja kwa moja ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.
Uhusiano na masuala mtambuko:
uraia: uzalendo – kushiriki katika kuimba wimbo wa taifa.
Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities na Movement and Creative Activities.
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kushiriki katika uskauti shuleni kupandisha bendera shuleni kushiriki katika kuimba wimbo wa taifa kuimba na kukariri mashairi kuhusu uzalendo.
Uhusiano na Maadili:
umoja, uzalendo, haki za kijamii, uwajibikaji, mapenzi kwa nchi, heshima na amani.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika kuimba nyimbo zinazokuza uzalendo katika sherehe mbalimbali.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
- kuchunguza anavyotumia msamiati wa shambani katika mawasiliano
- kuchunguza anavyotumia –ake na -ao katika mawasiliano
- kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kufuatilia mwandiko wake
- kuchunguza anavyotumia lugha katika masimulizi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti ipasavyo na kwa ufasaha
- anasimulia visa vinavyohusiana na uzalendo kwa ubunifu
- anasoma hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
- anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
- anatunga sentensi sahihi akitumia – ake na -ao kila wakati
- anaandika kisa kifupi kwa hati nadhifu, ubunifu, mtiririko mwafaka na kwa haraka.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti ipasavyo
- anasimulia visa vinavyohusiana na uzalendo
- anasoma hadithi kwa ufasaha
- anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- anatunga sentensi sahihi akitumia –ake na -ao
- anaandika kisa kifupi kwa hati bora na kwa mtiririko ufaao.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka baadhi ya sauti ipasavyo
- anasimulia visa vinavyohusiana na uzalendo.
- anasoma hadithi
- anafahamu baadhi ya hadithi aliyosoma na kusomewa
- ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akitumia –ake na -ao
- anajaribu kuandika kisa kifupi kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti ipasavyo
- ana changamoto katika kusimulia visa vinavyohusiana na uzalendo
- ana changamoto katika kusoma hadithi
- ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akitumia –ake na -ao
- ana changamoto katika kuandika kisa.