Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

 1. kutambua maneno yanayoonyesha uzalendo ili kuyatumia katika mawasiliano,
 2. kusimulia visa vinavyojumuisha  mambo yanayoweza kuimarisha

uzalendo ili kujenga stadi ya kuzungumza,

 • kusikiliza masimulizi kuhusu uzalendo ili kuimarisha usikivu,
 • kuthamini umuhimu wa uzalendo katika maisha ya kila siku. 

               MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

 • Mwanafunzi aeleze baadhi ya mambo yanayoweza kuimarisha uzalendo katika nchi yake kwa kutumia mgeni mwalikwa.
 • Mwanafunzi asimulie visa vinavyojumuisha mambo yanayoweza kuimarisha uzalendo kama vile amani, umoja, upendo na bendera ya Kenya.
 • Mwanafunzi asikilize kwa makini hadithi anazosimuliwa.  
 • Mwanafunzi aweza kutazama video inayoonyesha vitendo vya kizalendo.
 • Wanafunzi wajadiliane kuhusu uzalendo katika vikundi.
 • Wanafunzi waimbe wimbo wa taifa na kujadili maana ya baadhi ya maneno ya kizalendo katika wimbo huo.
 • Wanafunzi waimbe na kukariri mashairi kuhusu uzalendo.
 • Mwanafunzi atunge sentensi kuhusu baadhi ya mambo yanayohusu uzalendo.
 • Mwanafunzi ataje baadhi ya sifa za mzalendo kama vile kupenda nchi yake, amani na umoja.

MASWALI DADISi

 1. Je, ni nini maana ya uzalendo?
 2. Uzalendo una umuhimu gani?
 3. Je, ni kwa njia zipi unaweza kuonyesha uzalendo?
 4. Bendera ina umuhimu gani?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

uraia: uzalendo – kushiriki katika kuimba wimbo wa taifa mawasiliano na ushirikiano – kushirikiana pamoja darasani kufikiri kwa kina na kutatua matatizo – Katika kujibu maswali ya ufahamu yasiyo na majibu ya moja kwa moja ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

uraia: uzalendo – kushiriki katika kuimba wimbo wa taifa.

Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities na Movement and Creative Activities.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kushiriki katika uskauti shuleni kupandisha bendera shuleni kushiriki katika kuimba wimbo wa taifa kuimba na kukariri mashairi kuhusu uzalendo. 

Uhusiano na Maadili: 

umoja, uzalendo, haki za kijamii, uwajibikaji, mapenzi kwa nchi, heshima na amani.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika kuimba nyimbo zinazokuza uzalendo katika sherehe mbalimbali.

 Mapendekezo ya Tathmini:

 • kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
 • kuchunguza anavyotumia msamiati wa shambani katika mawasiliano
 • kuchunguza anavyotumia –ake na -ao katika mawasiliano
 • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
 • kufuatilia mwandiko wake
 • kuchunguza anavyotumia lugha katika masimulizi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka sauti ipasavyo na kwa ufasaha
 • anasimulia visa vinavyohusiana na uzalendo kwa ubunifu
 • anasoma hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
 • anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
 • anatunga sentensi sahihi akitumia – ake na -ao kila wakati
 • anaandika kisa kifupi kwa hati nadhifu, ubunifu, mtiririko mwafaka na kwa haraka. 

Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka sauti ipasavyo
 • anasimulia visa vinavyohusiana na uzalendo 
 • anasoma hadithi kwa ufasaha
 • anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
 • anatunga sentensi sahihi akitumia –ake na -ao 
 • anaandika kisa kifupi kwa hati bora na kwa mtiririko ufaao.

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka baadhi ya sauti ipasavyo
 • anasimulia visa vinavyohusiana na uzalendo.
 • anasoma hadithi
 • anafahamu baadhi ya hadithi aliyosoma na kusomewa
 • ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akitumia –ake na -ao 
 • anajaribu kuandika kisa kifupi kwa hati zinazosomeka.

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

 • ana changamoto katika kutamka  sauti ipasavyo
 • ana changamoto katika kusimulia visa vinavyohusiana na uzalendo
 • ana changamoto katika kusoma hadithi
 • ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
 • ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akitumia –ake na -ao 
 • ana changamoto katika kuandika kisa.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *