MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutaja vitu vinavyopatikana sokoni katika kuendeleza mazungumzo,
- kutaja watu wanaopatikana sokoni katika kuendeleza mazungumzo,
- kusikiliza maelezo kuhusu sokoni ili kujenga usikivu,
- kueleza shughuli zinazoendeshwa sokoni ili kuimarisha stadi ya kuzungumza,
- kueleza umuhimu wa soko ili kujenga stadi ya kuzungumza,
- kuthamini shughuli za sokoni kama njia moja ya kujipatia riziki.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi ataje vitu vipatikanavyo sokoni k.v.
mkokoteni, vibanda, ratili, bidhaa na risiti.
- Mwanafunzi ataje watu wanaopatikana sokoni kama vile dalali, mnunuzi, muuzaji na mchuuzi.
- Mwanafunzi ashiriki katika kuigiza michezo kuhusu shughuli zinazoendeshwa sokoni.
- Mwanafunzi ashiriki katika kujadili shughuli za sokoni.
- Mwanafunzi ajadili michoro, chati na picha kuhusu sokoni.
- Mwanafunzi atoe maelezo kuhusu umuhimu wa soko.
- Mwanafunzi aweza kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu shughuli za sokoni.
- Mwanafunzi aweza kutazama video na picha kuhusu shughuli za sokoni.
• Mwanafunzi asimulie kisa chochote alichoshuhudia kuhusu sokoni akiwa peke yake, katika kikundi au wakiwa wawili.
MASWALI DADISI
- Ni watu wepi wanaopatikana sokoni?
- Ni vitu gani vinavyopatikana sokoni?
- Soko lina umuhimu gani?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza hamu ya kuendeleza ujifunzaji – kusoma hadithi.
Uhusiano na masuala mtambuko:
elimu ya maendeleo endelevu: elimu ya masuala ya kifedha – kujadili umuhimu wa sokoni.
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji: kushiriki katika kuigiza shughuli za sokoni.
Uhusiano na Maadili:
uadilifu katika shughuli za sokoni umoja – Hamna biashara inayoweza kunawiri pasipo na umoja heshima ni muhimu popote watu wanapoingiliana hasa sokoni uwajibikaji – Mwenye biashara na mnunuzi sharti wawajibike katika shughuli husika.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kusaidia jamii katika shughuli zinazohusu soko.
Mapendekezo ya Tathmini:
• kuchunguza anavyotumia msamiati wa sokoni katika mawasiliano
- kuchunguza anavyotumia ndani ya na nje ya katika mawasiliano
- kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
- kufuatilia mwandiko wake.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua na kutumia msamiati unaotumika sokoni
- anasimulia visa kuhusu sokoni kwa ubunifu na ukakamavu
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu sokoni kwa ufasaha
- anatumia ndani ya na nje ya kutunga sentensi sahihi zenye ubunifu wa hali ya juu
- anaandika kisa kinachohusiana na sokoni kwa ubunifu, mtiririko, hati nadhifu na kwa kasi ifaayo.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua msamiati unaotumika sokoni
- anasimulia visa kuhusu sokoni kwa ukakamavu
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu sokoni
- anatumia ndani ya na nje ya kutunga sentensi sahihi
- anaandika kisa kinachohusiana na sokoni kwa mtiririko na hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua baadhi ya msamiati unaotumika sokoni
- anasimulia baadhi ya visa kuhusu sokoni
- anasoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu sokoni
- ana changamoto kiasi katika kutumia ndani ya na nje ya kutunga sentensi sahihi
- anaandika kisa kinachohusiana na sokoni kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutambua msamiati unaotumika sokoni
- ana changamoto katika kusimulia visa kuhusu sokoni
- ana changamoto katika kusoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu sokoni
- ana changamoto katika kutumia ndani ya na nje ya kutunga sentensi sahihi
- ana changamoto katika kuandika kisa kinachohusiana na sokoni.