Please Limited time Offer!

Familia ya mama yenye watoto watano iliishi nchini. Baba alitumikia jeshi na aliuawa katika vita. Katika Israeli, kuna sheria kwamba mmoja kati ya familia anapaswa kutumika katika jeshi. Sasa alikuwa mwana wa kwanza kujiunga na jeshi. Kwa bahati mbaya hata yeye aliuawa vitani.
Hilo liliendelea mpaka wana wote wanne wa familia hiyo wakauawa.

Sasa mama aliomba mwana wa tano na wa mwisho ajiunge na jeshi. Kwa hivyo alienda kwenye kamati ambako wataamua kuhusu kazi yake. katika kikao hicho, viongozi walisema “Ona tayari familia yako imeteseka sana. Wanafamilia yako wote wameuawa wakati wanatumikia jeshi. Kwa hivyo itakuwa bora ikiwa hautajiunga na jeshi”.

Basi mtoto wa tano ambaye alikuwa amedhamiria na kuamua kutumikia jeshini alijibu “Hapana bwana, niko tayari kutumika jeshini”.

Kwa hivyo walifanya mazungumzo kwa muda mrefu ili kutatua tatizo hilo. Viongozi walikuwa na nguvu sana kwa uamuzi wao. Hatimaye baada ya muda walifikia uamuzi kwamba

“Kwa vile mama yako ni mzee, twakuruhusu ukae na mama yako. Anakuhitaji. Baada yake kuaga dunia, tutakuruhusu uingie jeshini.”


Mwana alirudi nyumbani akiwa na uso wa huzuni na kumweleza mama hali hiyo. Yeye alitaka kujiunga na jeshi kusaidia nchi yake katika vita.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

One thought on “Kisa Kingine Cha Uzalendo -Grade 3”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *