Please Limited time Offer!

Siku moja msafiri alikuja kukutana na Chanakya. Alipofika nyumbani kwa Chanakya, jioni na giza ilikuwa imeanza kuingia. Msafiri alipoingia ndani, aliona kwamba Chanakya alikuwa na shughuli nyingi za kuandika chini ya mwanga wa taa ya mafuta (Kwa sababu wakati huo hapakuwa na umeme). Chanakya akitabasamu alimkaribisha mgeni na kumtaka aketi kisha akamaliza haraka kazi aliyokuwa akiifanya.

Mara tu baada ya kumaliza kazi hii. Chanakya alizima ile taa ya mafuta kisha akawasha taa nyingine.

Msafiri alishangaa kuona hivyo lakini alifikiri inaweza kuwa hii ni desturi inayofuatwa na wananchi wakati mgeni anafika.

Msafiri alipata udadisi na kuuliza, “Je, hii ni mila ya Nchi, mgeni anapofika nyumbani kwako?”

Chanakya aliuliza, “Mila gani?”

Msafiri akajibu, “Namaanisha kuzima taa moja na kuwasha taa nyingine?”

Chanakya akajibu, “Hapana, rafiki yangu mpendwa. Hakuna desturi hiyo. Kweli ulipoingia, nilikuwa nikifanya kazi rasmi, inayohusu, taifa langu.

Mafuta haya yaliyojazwa kwenye taa hii yalinunuliwa kutoka kwa fedha za Taifa. Lakini sasa, nazungumza na wewe. Haya ni mazungumzo ya kibinafsi, ya kirafiki, sio kazi yoyote inayohusiana na taifa langu. Kwa hivyo siwezi kutumia taa hiyo sasa, kwani itasababisha ufujaji wa pesa za taifa.

Kwa hivyo, nilizima taa hiyo na kuwasha taa hii nyingine, kwa kuwa mafuta kwenye taa hii yamenunuliwa kutoka kwa pesa zangu binafsi.

Kisa hiki kifupi kina tu funza ya kuwa Chanakya ni mzarendo. Hapendi kufuja pesa za nchi yake

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

3 thoughts on “Kisa Kifupi cha Uzalendo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *